16 October 2019
Mbeya boy X Dizasta vina X shaolin seneta _ Hasi na chanya lyrics
Mbeya boy
Napiga taya vibao stair ngumi chek mitindo, mapigo mabaya wote wako chini ya ulingo/
Nilivyosugu demu gani wakunivunja shingo, mistari tindo wako chini ya ukingo/
Nikisimama sioni mdada wakutamba, uliza wenzako nilichomfanya sholi mwamba/
Bila nguvu porini navuta kitu, moshi mwingi kama nachoma msitu/
Nazika marapa walijua mazishi, nilivyo kaligraph yo wakajua madishi/
Kichwani raga maphy nabugi nipo rumba, rip yangu kama choo kwaiyo nipo kila nyumba/
Cheza kibaiskel si unamiguu ya peda, mi nagonga demu yeyote hata akae kwenye zebra/
Rhymes sio matusi ila zinawachanganya, mfano we sio hesabu na nina uwezo wa kukufanya/
[Hook]
Mwalimu wa rap nakupa hesabu fanya, chukua hasi weka plus pata jibu gawanya/
Hapo inakua nini (hasi na chanya)x2
Dizasta vina
Eyo ticha nimesimama hayashime, natisha napo shika mic kama masai kashika sime/
Nawasha washa sasa imewaka nani azime, naokota tanga naua mwanza zika tarime/
Push rythems kama mjani man wanaelewa, mi na rap sana na ni kama dhambi niliyopewa/
Flani na flani wanaelewa hawataki tu kusema, sauti hewani mitaani sionekana kama hewa/
Dizasta vina ndio future yako, ni kijogoo uliyemkwepa mtaani halafu ukamkuta kwako....Mimi kama kumbukumbu ya torati, kutoka walawi, mwanzo, ayubu yohana, luka marko/
Kudadadeki hamnipi taji homie, maana huu ujio ni kama ford au bogi au radi homie/
Niko kitambo na sihitaji hodi, na wala sipingwi ka zinavyopingwa itikadi za kibabiloni/
Aah na mnapata uhondo nakili, mjeda nazalisha rhythms kama uoto wa asili/
Najua sana mwana inakupasa ukasome, hii waswahili wanaita mwana ukome/ dizasta
Mwalimu wa rap nakupa hesabu fanya, chukua hasi weka plus pata jibu gawanya/
Hapo inakua nini (hasi na chanya)x2
Shaolin seneta
Wananihoji eti hatari ni nini, njoo kwenye kiki ndio utajua hatari ni mimi/
Nikichana sina woga ila nawapa pressure, mpaka ma model na wanajiuliza wapi nimetoka/
Wabongo wananita black eminem, sifanyi soft wana wanajua nafanya black game/
Usinivute shati nyakati za mashaka, nina chale mwili mzima mcee utanichana wapi?/
Shaolin kisima cha verse kwa sasa, unaweza nita tajiri wa verse za mada/
y.o.u.n.g hauna swaga, ndani ya uwanja niko moto mpaka messi namanga/
Iwe kwa nguvu ya bia, au soda huwezi nidondosha nimesimama kama zakaria/
Matozi wana shine kwa kuazima, Hii ngoma ni nzito unaweza ukakonda ukiipima/
Mitaani wengi wananiogopa kama kifuku, adhabu kali ni kuweza kuicheza hii ngoma kiduku/
Nadhani kwa heshima na hasira, nikiona matozi wanachana truck bila vina/
[Hook]
Mwalimu wa rap nakupa hesabu fanya, chukua hasi weka plus pata jibu gawanya/
Hapo inakua nini (hasi na chanya)x2
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment